Story 1 | Simulizi 1

I honestly don’t remember the age at which I first found out about sex.

When I first got my period, I told my mother. She said that I was becoming a woman. I kind of already had an idea because I’d seen aunts and older cousins use sanitary products. There was no shame about nakedness, women just bathed and dressed in front of each other.

I was about 8 when my parents first spoke to me about sex. I was starting to get breasts and it was a short chat about some of the changes that would occur. There was no big talk. I grew up with and shared a room with older female cousins so I just knew that I would ultimately look like them. There were talks here and there about not messing with boys because that’s how you get pregnant or end up with HIV if you don’t use condoms.

Compared to what I’d heard elsewhere: like my other friends, I also learned about it from biology class and nurses who provided reproductive education in school. Some people learned from a designated lady in the village i.e. initiation school, who taught girls about womanhood etc.

Talking to future kids: Absolutely. I don’t intend to have one big talk because those are just awkward for everyone. I want to have regular conversations about these things.

, 28, Lesotho

(Go here to share your story!)

***

Kwa kweli sikumbuki nilikuwa na umri gani mara ya kwanza nilipofahamu kuhusu ngono.

Nilipovunja ungo, nilimwambia mama yangu. Alisema kuwa nimekuwa mwanamke. Tayari nilishahisi yanayohusika, kwa kuwa niliwahi kuwaona mama wadogo na mabinti zao wakitumia pedi na kadhalika. Hakukuwa na aibu kuhusu uchi, wanawake walioga na kuvaa kwa pamoja kwa uhuru.

Nilikuwa na miaka kama 8 wazazi wangu waliponiongelea kwa mara ya kwanza kuhusu ngono. Nilikuwa nimeanza kuota matiti na tuliongea kwa kifupi kuhusu mabadiliko yangeyotokea. Hakukuwa na hotuba kubwa. Nilikuwa nikilala chumba kimoja na madada zangu, hivyo nilijua kuwa hatimaye mwili wangu ungefanana na miili yao. Kulikuwa na maongezi hapa na pale kuhusu kutocheza na wavulana kwa kuwa hivyo ndivyo unavyoshika mimba au HIV kwa kutokutumia kondom.

Kulinganisha na yale niliyosikia kwingine: kama marafiki zangu, nilijfunza kwenye darasa la baiolojia na pia kwa manesi waliokuja shuleni kutoa elimu ya afya ya uzazi. Wengine walijifunza kwa mama aliyeteuliwa kijijini, yaani jandoni/unyangoni, aliyefundisha wasichana kuhusu kuwa mwanamke n.k.

Kuwafundisha wanangu huko mbeleni: Kabisa. Sinuii kuwa na kikao kwa kuwa muundo huo unamfedhesha tu kila mtu. Ninataka kuwa na maongezi ya kawaida kuhusu haya masuala.

, 28, Lesotho

(Nenda hapa ili kuchangia simulizi yako!)

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s